Mwanadada huyo ambaye kwa sasa anasomea taaluma ya saikolojia anasema kuwa aligundua talanta yake hiyo alipokuwa na miaka 12 alipokuwa ameenda kumtembelea mjomba wake aliyekuwa amekaribia kufa na ndipo aliponusa harufu mbaya ya mtu anayekaribia kufa ambayo hakuna mtu mwingine aliyeweza kunusa harufu hiyo.
“Nilidhani ni harufu ya mabaki ya mwili wa mjomba kwa sababu ilikuwa harufu mbaya sana ambayo sijawahi kuinusa. Lakini hakuna mtu mwingine aliyeweza kuinusa harufu hiyo” alisema Ari.
Ari aliongeza kuwa baadae alikuja kugundua kuwa mara kwa mara ameweza kunusa kifo na kuna wakati mwingine anaona ni mzigo kuwa na talanta hiyo na huwa anatamani kuwaambia watu wanaotaka kufa kwamba wanakaribia kufa lakini baadae huacha kwa sababu hilo sio jukumu lake.
Kwa sasa Ari Kala anawafundisha wanawake wenye umri kati ya 25-45 wanaotoka kwenye jamii zinazoamini uchawi kutumia vizuri talanta na vipaji vyao katika kuisaidia jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni