Ijumaa, 8 Juni 2018

LIGI KUU YA WANAWAKE YA 'SERENGETI PREMIUM LITE' KUENDELEA WIKIENDI HII



 Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya nane bora inatarajia kuendelea Jumamosi Juni 9,2018.


Ligi hiyo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars na baadaye timu ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens.

Viwanja vitatu ndivyo vitatumika kwa michezo hiyo ya wikiendi hii huku Uwanja wa Karume ukitumika kwa michezo miwili itakayochezwa saa 8 mchana na saa 10 jioni.

Evegreen vs Panama (Karume)
Alliance vs JKT Queens (Nyamagana)
Mlandizi Queens vs Baobab (Mabatini)
Simba Queens vs Kigoma Sisters (Karume)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni