mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Alhamisi, 7 Juni 2018
KOCHA MKUU SIMBA MWALIMU WA VIUNGO WATUPWA NJE YA KIKOSI WAKATI SIMBA IKIKIPIGA NA KK HOME BOYZ LEO
Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre pamoja na Mwalimu wa viungo, Aimen Habib, kwa pamoja watakosekana katika benchi la ufundi wakati Simba ikicheza dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC leo.
Katika orodha ya wachezaji na benchi la ufundi wa kikosi hicho iliyotoka punde inaonesha Kocha Msaidizi pekee, Masoud Djuma ndiye atakuwa anaiongoza Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Super Cup huko Kenya.
Haijajulikana sababu ya za kukosekana kwa wawili hao ni zipi ingawa imekuwa ikielezwa wamekuwa hawana mahusiano mazuri na kocha Msaidizi wa kikosi hizho.
Hivi karibuni kumezuka taarifa zinazoeleza kuwa Lechantre anaweza akatimkia Cameroon kwa ajili ya kutegemea kibarua cha kuinoa timu ya taifa hilo baada ya kutuma maombi ya kuomba kazi.
Aidha taarifa za ndani pia zinaeleza Lechantre na Aimen inawezekana safari ya kuitumikia Simba inaweza ikaishia baada ya michuano ya Super Cup kumalizika
CHANZO. SALEHE JEMBE BLOG.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni