mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumapili, 20 Mei 2018
YANAYOJIRI MKUTANO MKUU WA MABADILIKO SIMBA LEO
Mkutano Mkuu wa dharura wa Mabadiliko ya Kikatiba wa klabu ya Simba unatarajia kuanza hivi punde katika Ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Simba inaenda kufanya mabadiliko hayo ya katiba maalum kuupokea mfumo mpya wa kisasa wa uendeshaji wa klabu hiyo.
Ikumbukwe Simba walitumia miaka takribani miwili kwa ajili ya mchakato wa mabadiliko na mwisho mshindi wa zabuni alipatikana ambaye ni Mwanachama na shabiki wa timu hiyo, Mfanyabiashara na bilionea Mohammed Dewji 'Mo'.
Mkutano huo unaenda kupokea rasmi mfumo huo mpya na wa kisasa kwa ajili ya klabu hiyo kujiwekeza zaidi kibiashara na kuachana na huu wa zamani unaotegemea ada za wanachama.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni