
Nchi wanachama wa mkutano wa shirika
la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni
suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia
Maelfu
ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu
inayotokana na shambulio la nyoka.WHO inasema athari zinazotokana na
kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki
ambayo hayatiliwi maanani.kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO , kuna nia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka.
Nyoka agunduliwa ndani ya mkebe wa chakula cha mtoto Australia
Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema kuwa hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote.
Shirika la Afya duniani sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha.hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa ambazo ilikua gharama kupatikana kwenye nchi zilizo masikini hasa zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

Hali ya umasikini na kutokuwa na vituo vya afya vinavyokidhi mahitaji kumesababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wakitafuta tiba kwa matabibu wa kienyeji ambao husababisha madhara zaidi.
Lakini mpango huu mpya utalenga kuwafundisha watoa huduma wa afya jinsi ya kushughulikia mtu aliyeumwa na nyoka na elimu ya huduma ya kwanza kwa jamii iliyo hatarini.
Kila mwaka zaidi ya watu laki moja hufa duniani kutokana na kuumwa na nyoka asilimia 20 kutoka barani Afrika.Karibu watu nusu milioni wana ulemavu wa kutokuona, kukatwa viungo na ulemavu mwingine kutokana na mashambulizi ya nyoka.
Dondoo za huduma ya kwanza baada ya mtu kuumwa na nyoka:
- Jaribu kukumbuka umbo na rangi ya Nyoka:
- Ondoka eneo la hatari
- Usifyonze sumu kutoka kwenye jeraha
- Ondoa vitu vilivyovaliwa sehemu iliyoathiriwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni