Taarifa ya shirika la Habari la BBC, inaeleza kuwa Richard Mboyo Iluka, Naibu Gavana wa jimbo la Tshuapa amesema kuwa boti hilo ilikuwa imewabeba abiria wengi, wengi wao wafanyabiashara waliokuwa wanasafiri kutoka eneo la Monkoto kwenda Mbandaka.
Amesema watu wengine 50 wamenusurika. Gavana huyu amesema hadi sasa hawajafahamu chanzo cha ajali hiyo.
Kwa sasa maafisa wakuu wa jimbo hilo wamesafiri kwenda eneo la ajali kufahamu zaidi kuhusu idadi rasmi ya waliofariki na watu ambao walikuwa ndani ya boti hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni