Timu zilizotajwa kushiriki michuano hiyo kutoka Tanzania ni Simba SC, Yanga SC, Singida United na JKU ya Zanzibar wakati Kenya yenyewe ikitoa jumla ya timu nne ambazo ni Gor Mahia, FC Leopards, Kaliobangi Sharks na Kakamega Home Boys.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2018 atapata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na Everton FC ya England katika uwanja wa Everton uliyopo jijini Liverpool nchini England ukijulikana kwa jina la Goodson Park, inaaminika kama timu ya Tanzania itatwaa taji hilo hiyo itakuwa ni fursa kwa wachezaji wao kuonesha uwezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni