mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania
blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla
kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumamosi, 26 Mei 2018
Sasa Ukipoteza Passport utatozwa Laki 5 hadi 7 kupata mpya
Kamishna wa Uhamiaji, Uraia na Passport, Gerald Kihinga amesema
Mtanzania atakayepoteza hati ya kielektroniki ya kusafiria inayopatikana
kwa Shilingi 150,000 atalazimika kulipa Shilingi 500,000 kupata mpya.
Pia aliongeza kuwa iwapo ataipoteza tena hiyo aliyoipata kwa Tsh. 500,000 basi atalipa Tsh. 750,000 ili aweze kupata nyingine.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa utoaji wa hati hizo ambapo tayari hati
15,101 zimeshatolewa kwa Watanzania tangu kuanza kwa utoaji huo January
mwaka huu.
Kihinga amesema zipo kesi nyingi za watu kupoteza hati zao za kusafiria
na baadhi yake ni zile zinazotokea katika matukio yasiyohitaji uwapo
wake hati hizo hivyo gharama hiyo itasaidia watu kutunza hati zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni