Ijumaa, 4 Mei 2018

RAIS MAGUFULI ZIARANI MOROGORO:

Image may contain: one or more people, eyeglasses and closeup

 Rais Magufuli alipompigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo mara baada ya kulalamikiwa kuhusu kero ya maji katika eneo la Kidodi Kilombero.
Rais Magufuli amemuagiza Prof Kitila kufika hapo mara moja kushughulikia kero hiyo.
Ametoa agizo hilo baada ya kusimamishwa na wananchi katika kijiji hicho cha Kidodi na kumlalamikia kuhusu kero ya maji ambayo inadaiwa kuwa kuna mradi ambao umekwamishwa na mkandarasi.
Rais Magufuli amesema tayari mkandarasi huyo alikwishapewa fedha zaidi ya shilingi milioni 800 ambapo amesema "Kama alikula hiyo hela, atazitapika"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni