Real Madrid wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Liverpool na kufanikiwa kutetea taji lao la UEFA Champions League kwa mara ya tatu mfululizo, magoli ya Real Madridi yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 51 na Gareth Bale aliyefunga magoli mawili dakika ya 64 na 83, goli pekee la Liverpool lilifungwa na Sadio Mane dakika ya 55.
Ushindi huo sasa unaifanya Real Madrid kuwa timu ya kwanza kuwahi kutwaa taji la UEFA Champions Leagu mara tatu mfululizo wakati Cristiano Ronaldo hilo linakuwa ni taji lake la tano la UEFA Champions League katika maisha yake na ndio mchezaji pekee aliyeshinda taji hilo mara tano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni