Leo May 19, 2018 Imethibitishwa kuwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli atashiriki katika zoezi la kupokea Kombe
la Ubingwa wa CECAFA pamoja na kuwakabidhi kombe la mabingwa wa michuano
ya ligi kuu soka Tanzania Bara mabingwa wapya Simba SC.
Kupitia ukurasa wa
Twitter wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa
amesema Rais Magufuli ataungana na wanamichezo katika uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam.
“Rais
Magufuli leo ataungana na wanamichezo kupokea kombe la ubingwa wa
CECAFA kutoka timu ya Serengeti Boys, kuipokea timu ya TSC iliyoibuka
mabingwa wa pili wa dunia huko Urusi na kukabidhi kombe kwa Mabingwa wa
Ligi Kuu Tanzania Bara, uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa
8 mchana” amesandika Msigwa.Tukio hili la kimichezo ni kwa Rais Dkt. Magufuli ndio la kwanza kulifanya tokea alipoingia madarakani na hivyo atakuwa amewawekea historia kubwa klabu ya Simba SC kukabidhiwa kikombe na Rais pamoja na Serengeti Boys.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni