
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa
matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa
taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi
kutumiwa nchini Korea Kaskazini.
Pendekezo la John Bolton
liliighadhabisha na kuitia wasiwasi Korea Kaskazini ambayo ilitisha
kujitoa kwa mkutano na Trump wa mwezi ujao.Bw Trump amesema anaamini mkutano huo utafanyika.
Mwaka 2003 kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ili apate kuondolewa vikwazo na mataifa ya Magharibi.

Hata hivyo aliuawa na waasi walioungwa mkono na nchi za Magharibi miaka kadhaa baadaye, mfano ambao ulionekana kumtia wasi wasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Pyongyang ilionya Jumatano kuwa huenda isihudhurie mazungumzo hayo ambayo yanapangwa kufanyika nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni.
Rais Trump alisema nini?
Huku Bolton akitazama, Rais Trump alisema: "Mfumo wa Libya si mfumo tuko nao kabisa wakati tunafikiri kuhusu Korea Kaskazini."Makubaliano ambayo Bw Trump alikuwa akizungumzia na Kim Jong-un ni kitu ambacho Kim atakuwepo, atakuwa nchini mwake, ataiongoza nchi yake na nchi yake itakuwa tajiri sana.
Ukiangalia Korea Kusini, huu utakuwa mfumo sawa na wa Korea Kusini kimaendeleo... ni watu wanaojitahidi sana."
Kuhusu mkutano uliopangwa, Trump alisema: "Hakuna kilichobadilika na Korea Kaskazini tunachokifahamau, hatujaambiwa chochote."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni