Jumanne, 22 Mei 2018

BAADA YA MIAKA 12, MTOTO AZALIWA

Image may contain: cloud, sky, ocean, outdoor, nature and water

 Kisiwa kimoja nchini Brazil ambacho ni marufuku kwa mwanamke kujifungua kinasherehekea mtoto wa kwanza kuzaliwa kisiwani humo katika kipindi cha miaka 12.

Kisiwa cha Fernando de Noronha kinachopatikana kilomita 370 kutoka mjini Natal, kina wakazi takriban 3,000 lakini hakijawahi kuwa na hospitali za kujifungulia wala wajawazito.

Wanawake wanaotaka kujifungua katika kisiwa hicho hutakiwa kusafiri hadi bara.

Kuhusu mwanamke huyo mwenye miaka 22 ambaye hakutaka jina lake litajwe aliyejifungua mtoto wa kike Jumamosi kisiwani humo, amesema hakufahamu kwamba alikuwa mjamzito wakati wote.

Ijumaa usiku nilianza kuhisi maumivu na nilipokwenda kwenye bafu nikagundua kitu kikitoka kupitia miguu yangu," amenukuliwa na tovuti ya O Globo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni