Jumamosi, 10 Machi 2018

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson augua akiwa Kenya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson, ambaye amesafiri hadi Kenya katika ziara yake barani Afrika amefuta mikutano yote katika siku ya kwanza yake Kenya.

Hii ni kutokana na Tillerson kuugua siku ya kwanza akiwa Kenya.

Kwa mujibu wa habari,hali hiyo imekuja baada ya kuwa Tillerson ametumia nguvu nyingi katika masuala muhimu kama Korea Kaskazini.

Taarifa zinasema kuwa hali ya Tillerson sio mbaya na hivyo mipango iliyoahirishwa inaweza kufanyika siku zinazofuata.

Tillerson amewasili Kenya baada ya kufanya ziara Ethiopea.

Baada ya Kenya,waziri huyo ataeleka Djibouti,Chad na Nigeria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni