Wastara amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, Wastara anasema kuwa alimuandikia barua Diamond Platnumz kuomba msaada pamoja na Alikiba lakini kwa Diamond alionekana yeye ni kama tapeli.
"Niliandika barua kuomba msaada hivyo nilimuandikia Diamond lakini watu wake walimfikishia taarifa kuwa mimi tapeli hivyo hakuweza nisaidia ila pia wakati huo huo nilimuandikia Alikiba na Alikiba akaniambia kuwa kuna watu walikuwa na show yao Kenya ila walikuwa hawana fedha yeye anazohitaji hivyo akaniahidi kuwa atakwenda kufanya show hiyo ili aje kunisaidia, kweli alikwenda na aliporudi aliniletea fedha hizo" alisema Wastara.
Mbali na hilo Wastara amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni