Leo March 2, 2018 baadhi
ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo wametangaza
rasmi kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Kati ya waliohama ni pamoja na Katibu na Katibu Mwenezi wa Jimbo la
Ubungo.Wamedai kuwa kwasasa chama hicho kina hali mbaya kwani hawajui
kipi kati ya uadilifu, uwajibikaji na umoja unatekelezwa sawia.
Viongozi hao wameelezwa kusikitishwa na kitendo cha Kiongozi wao
mkubwa Zitto Kabwe kushinikiza viongozi wa CHADEMA wafanye maamuzi kwani
serikali hii ni rahisi sana kuiangusha.
“Kwa
pamoja tunatangaza kujivua uanachama, na kujiunga na CCM kwa maana ya
kusimamia misingi ya chama ambayo ilishindwa kutekeleza, lakini leo Rais
aliye madarakani na serikali wameanza kuirudisha misingi ambayo
tuliipigania tukiwa ACT Wazalendo.” – Kiongozi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni