Wadau wa elimu wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamekuwa na
mtazamo tofauti juu ya agizo la Rais Magufuli kufuta michango kwa
wanafunziwa shule za msingi na sekondari, huku miundombinu ya shule
nyingi mkoani humo ikiwa si ya kuridhisha jambo lililosababisha
wanafunzi zaidi ya 1553 kukosa nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato
cha kwanza mwaka huu.
Wadau hao wamesema kuwa tamko la rais halikuzingatia Jografia ya maeneo ya pembezoni
mwa nchi kama vile mkoa wa Rukwa. Walidai kuwa ili kuinua hadhi ya
elimu ambayo imekuwa nyuma tangu uhuru, ushiriki wa wananchi hauepukiki.
“Ni kweli serikali imetoa zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya maendeleo
ya elimu katika manispaa yetu, lakini fedha hizi ni tone ukilinganisha
na matatizo tuliyo nayo. Haziwezi kutatua kila changamoto tulizonazo.
hivyo basi michango ya wadau na wazazi haiepukiki,” Zeno Nkoswe mdau wa
elimu manispaa ya Sumbawanga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni