Homa ya Lassa sio ugonjwa mpya, lakini huzuka mara chache na ukizuka husambaa haraka na kwenye eneo kubwa kuliko siku za nyuma na kuenea kwa kasi zaidi na zaidi kuliko hapo awali.
Inakadiriwa kuwa mpaka sasa watu 90 wameshafariki kutokana na ugonjwa huo lakini inahisiwa kuwa idadi ya vifo inaweza kuwa juu zaidi kuliko inavyojulikana kwasababu ugonjwa huo unaelezwa kuwa mgumu sana kupimwa na kugundulika.
Wanawake wajawazito ambao wanakaribia kujifungua wakipata ugonjwa huu wanakuwa kwenye hatari ya asilimia 80 kupoteza watoto wao au wenyewe kufariki.
Katika hatua za mwazo za ugonjwa huu inaelezwa kuwa vigumu kupimwa na kujulikana kwani huwa kama magonjwa ya Malaria na Dengue.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni