Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Habari nchini kutambua kuwa utoaji wa habari kwa wananchi kwa sasa siyo utashi tena bali ni sheria.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo, Jumatatu, jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa habari kwa mwaka 2018, ambacho kimebeba kauli mbiu isemayo, " Je, Mawasiliano ya Kimkakati Yanachagiza vipi Tanzania ya Viwanda?
Waziri Mwakyembe amesema kwa sasa Tanzania inahitaji Afisa Habari anayejituma, anayehuisha tovuti yake na kuwa na uhusiano mzuri na vyombo vya habari vinavyomzunguka.
"Serikali
inatarajia kuwa maafisa mawasiliano serikalini mtakuwa wabunifu na
kuwapatia wananchi haki yao ya msingi ya kupata taarifa". alisema
Waziri Dkt. Mwakyembe.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni