Ijumaa, 16 Machi 2018

TFDA YAAGIZWA KUDHIBITI UBORA WA DAWA ZA MENO


Wakati Tanzania ikijiandaa kuadhimisha siku ya kinywa na meno, Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndungulile ameagiza mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA kuchukua hatua stahiki za kuhakikisha wanafanya msako mkali wa kudhibiti uingizwaji wa dawa za meno zisizo na ubora nchini.

Naibu waziri ndugulile ametoa agizo hilo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na agizo hilo pia amewataka kupunguza matumizi ya vileo na tumbaku kutokana na athari kubwa zinazojitokeza katika afya ya kinywa na meno.

Maadhimisho hayo hufanyika Machi 20 kila mwaka, na mwaka huu kitaifa yamepangwa kufanyika wilayani Tarime mkoani Mara yakiwa yamebaba kauli mbiu isemayo “sema haaaaaa fikiri kinywa fikiri afya’’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni