Maduka ya supermarket
nchini Afrika Kusini hivi karibuni wameanza kuondoa kwenye maduka hayo
soseji ambazo zimepigwa marufuku nchini humo kutokana na kudaiwa
kuwa soseji hizo zina sumu baada ya kusababisha vifo vya watu 180.
Serikali imeeleza kuwa soseji
hizo zina sumu aina ya listeria hivyo kutoa onyo kwa raia wake kuepuka
kula nyama za aina zote ambazo zimeshatengenezwa na ziko tayari kuliwa
tu. Wateja waliokuwa wamenunua soseji hizo wamezirudisha huku wengine
wakihitaji pesa zao zirudishwe.
Inaelezwa kuwa madhara yaliyosababishwa na soseji hizo
yamegundulika baada ya kuathiri watu wengi katika kipindi cha mwaka
mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni