Ijumaa, 9 Machi 2018

Refa wa Afrika Mashariki amechaguliwa kuchezesha World Cup 2018

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeonesha kuzidi kuwaamini marefa wa Afrika baada ya refa Aden Marwa Range kutokea Ligi Kuu Kenya kuchaguliwa kwenda kuchezesha Kombe la Dunia.

FIFA imetangaza kumchagua Aden Marwa Range kwenda kuchezesha Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kama muamuzi msaidizi katika michuano hiyo.
Maamuzi hayo ya FIFA yanazidi kuleta matumaini katika soka la Afrika upande wa waamuzi, kwani yanaonesha waamuzi wa Afrika kuzidi kuimarika, Michuano ya Kombe la Dunia 2018 itachezwa kwa mwezi mmoja nchini Urusi kuanzia June 14 – July 15 2018.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni