Nahodha wa klabu ya Fiorentina na mchezaji wa timu ya taifa ya
Italia, David Astori amefariki dunia usiku wa kumamkia leo huko mjini
Udine nchini Italia akiwa hotelini akisubiri mchezo wa leo dhidi ya
klabu ya Udinese.
Gazeti la Udine Today mapema leo asubuhi Jumapili Machi 4, 2018
limesema mchezaji huyo alishindwa kuamka hadi saa tatu na ndipo wahudumu
walipolazimika kufungua mlango kwa nguvu na kumkuta akiwa tayari
ameshafariki.
Mtandao wa klabu ya Fiorentina nao umeandika taarifa iliyosomeka
“Tunasikitika kutangaza kwamba nahodha David Astori amefariki, kwa hali
hii ya kutisha na ya kushangaza, na juu ya yote kutokana na heshima kwa
familia yake tunaomba utulivu kwaajili ya taarifa zaidi’,”.
Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi juu ya kifo hicho kutoka kwa jeshi la polisi.
Kufuatia msiba huo,Shirikisho la Soka nchini Italia (IFF) limetangaza
kusogeza mbele mechi 7 za leo ambazo nyingine zilitarajiwa kupigwa
mchana huu.
David Astori (31) alijiunga na Fiorentina mwaka 2015 akitokea
Cagliari ambapo awali alimpelekwa kwa mkopo AS Roma na kisha kununuliwa
moja kwa moja na Fiorentina, ambapo hadi mauti yanamkuta alikuwa
ameshacheza mechi 90 na kutupia magoli matatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni