Jumamosi, 10 Machi 2018

Kubenea akabidhi ofisi

Baada Mkuu wa wilaya Ali Hapi kumfukuza kwenye Ofisi yake ya ubunge iliyokuwa katika manispaa ya Kinondoni Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amefunguka na kusema kuwa ameondoa nyaraka zake na kukabidhi ofisi hiyo.

Kubenea amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kinondoni na kusema kitendo hicho ni kujitafutia ujiko kwa wakubwa wake wa kazi ili apandishwe cheopia amebainisha kuwa kwa sasa umezuka mtindo kwa watumishi wa umma kugombana na wabunge wa upinzani ili wapandishwe vyeo.

Ameongeza kuwa ni kweli amefukuzwa katika ofisi hizo na kwamba tayari  ameshapata ofisi nyingine katika eneo la ubungo maeneo ya majengo ya urafiki.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Happi aliwafukuza katika ofisi zao wabunge wote waliokuwa wakitumia jengo la mkuu wa wilaya kwa madai kuwa anataka kuzitumia ofisi hizo kwa matumizi ya serikali.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni