Serikali ya Tanzania kupitia kwa msemaji wake, Dkt. Hassan Abbas
amechukua hatua ya kuwaita wamiliki wa gazeti la Tanzanite ambalo
linatoka mara moja kwa wiki (Jumatatu) baada ya kupokea malalamiko mengi
kutoka kwa wananchi kutokana na ukakasi wa habari zake.

Mange Kimambi
Dkt. Abbas ametoa taarifa hiyo ya wito kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “
Nimepokea
malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma katika toleo linaloonekana
mtandaoni la gazeti la Tanzanite. Gazeti hili limesajiliwa kutoka kila
Jumatatu. Hivyo tumewaita wahusika kesho baada ya kuona nakala halisi
ili kupata maelezo yao.“.
Moja ya nakala ya gazeti hilo inayoonekana kusambaa kwenye mitandao
ya kijamii iliyochapishwa Jumatatu ya wiki hii ina baadhi ya vichwa vya
habari vinavyosomeka.
“Mbowe ameanza kuchanganyikiwa au ameamua kuudanganya umma?”, “Kila
mwanaume ana tezi dume” “Hawa ndio Maadui wakubwa wa serikali ya JPM”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni