Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) mkoani
Shinyanga kimelaani vikali kitendo cha Diwani wa Kata ya Bunambiu
wilayani Kishapu, Richard Sangisangi cha kumshambulia kwa kumpiga
muuguzi wa Kituo cha Afya cha Kata hiyo, Hilda Simon wakati akitekeleza
majukumu yake.
Mwenyekiti wa TUGHE mkoani Shinyanga, John
Mfutakamba amesema kitendo cha diwani huyo kumpiga muuguzi huyo msaidizi
mbele ya wagonjwa akitekeleza wajibu wake ni cha kumdhalilisha na
litamtesa kisaikolojia na kuitaka jamii kukikemea kwa nguvu zote maana
kinawavunja moyo watumishi wa umma.Hilda Simon ni Muuguzi Msaidizi wa Kituo cha afya cha Kata ya Bunambiu anasema alipokea kipigo kutoka kwa diwani huyo akimtuhumu kutoridhishwa na huduma anayoitoa kwa wagonjwa ikiwa ni maelezo aliyoyapata kwa ndugu za wagonjwa kwa njia ya simu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni