Alhamisi, 8 Machi 2018

chuo kikuu mzumbe chaadhimisha siku ya wanawake duniani kisomi



chuo kikuu cha mzumbe kampasi kuu , ya mkoani morogoro leo wameungana na ulimwengu kuadhimisha  siku ya wanawake duniani hii leo kwa aina yake kwakushirikisha  wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi wanazunguka chuo hicho.

katika maadhimisho hayo   yaliyoambatana na  maandamano. ya wanafunzi na wakufunzi wa chuo hicho ambapo pia mada mbalimbali ziliwasilishwa na maprofesa wa chuo hicho ikiwa ni kuwajengea uwezo  wanafunzi shule hizo  kujituma katika masomo na kufikia malengo yao.


mbali na matukio hayo  uongozi wa chuo cha mzumbe umechangisha fedha takribani milioni 2 kusaidia ujenzi wa choo katika shule ya msingi mzumbe inayokabiliwa na changamoto hiyo.pamoja na kuzindua mpango  wa kutoa elimu mbalimbali za ujasiriamali   kwa vijiji vya jirani vinavyoizunguka chuo hicho nawilaya ya mvomero kwa ujumla.










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni