Jumamosi, 10 Machi 2018

BABU WA MIAKA 79 AACHA SHULE, AKISEMA HAELEWI MASOMO YAKE


Safari ya elimu ya Mzee Nyamohanga Suguta mwenye umri wa Miaka 79 ambaye mwaka jana alianza masomo ya darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Makerero wilayani Tarime Mkoani Mara imeshindwa kufanikiwa baada ya Mzee huyo kuacha shule akisema haelewi masomo yake.


Nyamhanga Suguta (79) mkazi wa kijiji cha Getenga kata ya Mbogi
wilaya ya Tarime mkoani Mara akiwa ndani ya darasa la kwanza katika
shule ya msingi Makerero baada ya kuamua kuanza kusoma ili kujua
Kuhesabu, Kuandika na Kusoma Mwaka jana kabla ya kuacha Masomo .

 Nyamhanga Suguta (79) mkazi wa kijiji cha Getenga kata ya Mbogi
wilaya ya Tarime mkoani Mara akiwa  Nyumbani kwake baada ya kutembelewa
ili kujua kwanini ameamua kuacha shule bila ya kutimiza
ndoto zake za kujua kusoma , kuhesabu na Kuandika ili aweze kurudishia
vizuri chenji kama alivyodai hapo awali Mwaka jana. 

Shule
ya Msingi Makerero aliyokuwa akisoma Mzee huyo lakini Mwalimu Mkuu
Msaidizi wa Shule hiyo Mwl: Kenedy Wayoga amesem akuwa tangu shule hiyo
kufunguliwa mzee huyo hajawahi kwendea shuleni hapo baada ya kuwa
anasoma Mwenyewe pale wanafunzi wanapoondoka kwenda Nyumbani kwao, Mzee
huyo alianza Darasa  la kwanza Mwaka Jana ili aweze kujua Kusoma ,
Kuandika na Kuhesabu kwa lengo la Kuendeleza biashara zake za kuuza
Ndizi kijijini hapo.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni