Afande Sele ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa kuna wasanii wa hip hop ambao alitegemea wangekuja kuendeleza muziki huo vizuri lakini ndio wamekuwa viongozi katika kuimba matusi.
“Wasanii wa sasa hivi wanaimba nyimbo za mapenzi, ngono, kubakana, pombe, ndoa kuvunjika, mambo ya kunajisiana,” amesema.
“Nasikitika sana kuona baadhi ya wasanii ambao nilijua watakuja kuwa waridhi wetu kwenye vipaji vya hip hop, wamebadilika leo ndio wanaimba matusi ya kijinga,” amesisitiza.
Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilimfungia kwa miezi sita msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki kutojihusisha na shughuli zozote za sanaa baada ya kukaidi agizo la kubadilisha maudhi ya wimbo wake wa Kiba_100.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni