Jumatano, 14 Februari 2018

ZUMA AWAJIBU ANC:

Image may contain: one or more people, night and closeup


Rais wa Afrika kusini anayeandamwa na kashfa, Jacob Zuma ameibuka na kusema kuwa hajafanya lolote baya na haoni sababu ya kuondoka haraka katika nafasi yake hiyo.

Zuma amesema hayo baada ya Chama chake cha African National Congress (ANC) kutangaza kuwa itakwenda kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye, kesho Alhamisi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 amekuwa kwenye shinikizo kubwa la kumtaka kujiuzulu kutokana na madai mengi ya kuhusishwa na rushwa.

Akizungumza Zuma amesema: "Siyo haki na sawa kwangu katika suala hili lililoibuliwa," alikiambia Kituo cha runinga cha SABC wakati wa mahojiano marefu ambayo hayakutangazwa. "Hawakuweza kunipatia sababu zozote."

Zuma amesema, muda wake wa kuondoka ni hadi mwezi Juni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni