
Yaya mmoja nchini Malaysia ambaye alidhulumiwa na mwajiri wake kwa kumlazimisha kulala nje na mbwa amefariki dunia
Yaya huyo kwa jina Adelina alitokea nchini Indonesia na kwenda kuifanyia kazi familia moja huko Panang, Malaysia.Waajiri wake wanalaumiwa kwa kutompa chakula na kutojali kuwa vidonda vyake vingepata matibabu.
Adelina aliokolewa tarehe 10 Februari baada ya jirani kuripoti hali yake kwa mwanasiasa Steven Sim.
Alilazwa hospitalini siku ya Jumapili ambayo alifariki dunia baadaye.
Mwanamke wa umri wa miaka 36 na nduguye kwa sasa wanachunguzwa kwa kushukiwa kuua kwa mujibu wa polisi wa Malaysia.
Mama yao wa miaka 60 pia amekamatwa na kwa sasa yuko kwenye kizuizi cha polisi.

Inaripotiwa kuwa Adelina alikuwa na vidonda na hakuwa ametibiwa hali ilichangia kufeli kwa viungo vya mwili.
Waziri wa mashauri ya chi kigeni wa Indonesia Ratno Marsudi alisema alitaka Adelina apate haki.
Malaysia ni moja ya nchi zinazowachukuaa wafanyakazi wengi zaidi Asia ambapo wafanyazi uhamia huko kufanya kazi na malipo ya chini.
Kuna takriba raia milioni 2.5 wa Indonesia wanaofanya kazi nchini Malaysia na nusu yao wanafanya kazi kinyume cha sheria.
Wafanyakazi wengine hutokea nchini za Myanmar, Ufilipino, Vietnam, Bangladesh, Laos, Cambodia, Sri Lanka na Thailand.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni