Amechukua
hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake
ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vema halmashauri hiyo na
kuisababishia hasara ya Milioni 279.
Waziri
Mkuu amemsimamisha kazi Sebukoto leo wakati akizungumza na watumishi na
madiwani wa halmashauri hiyo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya
kikazi mkoani Mwanza.
“Mwanasheria
utasimama kazi kuanzia leo na tuhuma zako zitachunguzwa kikamilifu na
vyombo husika na uchunguzi ukibaini kama huna kosa utarudi kazini.
Hatuta kuonea lakini hatuwezi kukuvumilia kwa utaratibu huo ulioufanya.”
–Majaliwa
Waziri
Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na
matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema fedha
alizolipwa Bahebe zingeweza kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali
ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni