Wafanyakazi wa majumbani jijini Nairobi wameandamana wakitoa wito kwa serikali kuwatambua kama wafanyakazi wengine ili pia wao waweze kupata manufaa ya ajira kama vile bima ya afya, likizo ya uzazi na malipo ya uzeeni
Imedaiwa kuwa mfanyakazi wa nyumbani anapokuwa mgonjwa, jambo la kwanza mwajiri hufikiria kumfukuza.
Hata hivyo kwa sheria za nchini Kenya, wafanyakazi wa nyumbani wana na haki sawa na mfanyakazi mwingine yeyote.
Kwa mujibu wa sheria hizo, iwapo mfanyakazi wa ndani ataugua, ana haki
ya kutibiwa na pia ana haki ya likizo ya kila mwaka isiyopungua siku 21.
Kisheria, waajiri wanatakiwa kuchangia malipo ya bima ya afya na hazina ya malipo ya uzeeni.
Sheria hii ikipitishwa Tanzania, je itatekelezeka kirahisi?
Kisheria, waajiri wanatakiwa kuchangia malipo ya bima ya afya na hazina ya malipo ya uzeeni.
Sheria hii ikipitishwa Tanzania, je itatekelezeka kirahisi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni