
Kikosi cha Simba kuanza mazoezi kesho kujiandaa na Mbao FC
Kikosi cha Simba kesho jioni kitaanza tena mazoezi tayari kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Mbao FC.
Kikosi cha Simba kilipewa mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Djibout katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gendarmerie ambapo kikosi cha Simba kilishinda kwa goli 1-0 na hivyo kujiandikishia tiketi ya kwenda hatua ya mbele zaidi.
Mazoezi kesho jioni yataanza saa 10:00 katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni