Jumatatu, 12 Februari 2018

Ndege yenye abiria 71 imeanguka nchini Urusi

Stori inayoshika headlines kimataifa leo February 11, 2018 ni kuhusiana na ajali ya Ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na wahudumu  imeanguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa ndege mjini Moscow.
Ndege hiyo ya shirika la Saratov ya An-148, ilikuwa safarini kwenda mji wa Orsk wakati ilipopoteza mawasiliano.
Huduma za dharura ziliambia vyombo vya habari kuwa ndege hiyo ilianguka na hakuna uwezekano wa kuwapata manusura, inaripotiwa kuanguka karibu na Argunovo Kilomita 80 kusini mashariki mwa Moscow.
Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni