Msimu
wa mafua makali tayari umebidha hodi katika nchi kadhaa huku
ukinyemelea mataifa mengine, limesema shirika la afya duniani, WHO.
Kutokana
na hali hiyo WHO imetoa mwongozo wa kuzingatia wakati wa msimu huu wa
mafua makali ambapo baadhi ya nchi zimepata idadi kubwa zaidi ya
wagonjwa.
Nchini Marekani viwango vya wanaokwenda hospitalini kutibiwa mafua ni sawa na vile vilivyotokea misimu saba iliyopita.
Maeneo ya tropiki kama vile barani Afrika, taarifa za visa vya mafua zimeripotiwa katika nchi kama vile Madagascar, ilhali bara la Asia nchi za Pakistan na Singapore ndiyo zinaongoza.
Kwa mantiki hiyo WHO imependekeza nchi ambazo tayari zinakabiliwa na ugonjwa huo kupatia chanjo makundi ambayo yanakabiliwa zaidi na mafua hayo.
WHO inasema njia bora ya kuzuia mafua hayo ni chanjo ambapo hutolewa kabla ya kuanza kwa msimu wa ugonjwa huo na inashauriwa mtu apatiwe chanjo kila mwaka kwa sababu kila mara virusi vya mafua hubadilika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni