kwani wanyama hawa ni Mbwa mwitu ni
wanyama wawindaji wanaokula nyama, ni wanyama wafupi na wadogo kimuonekano,
huishi katika makundi makumbwa sana, urefu wa kutoka miguuni hadi begani huweza
kufikia inches 35 tuu na hiyo ni kwa wale ambao wakubwa, lakini urefu wa
kichwani mpaka mkiani hufikia inches 55, kwa vipimo hivi unaweza kuona wanyama
hawa ni wadogo kiasi gani kwa maumbo yao, lakini kama vipimo hivyo ni mtihani
basi kukurahisishia nakwambia hivi, mbwa mwitu kwa umbo ni mdogo zaidi kwa mbwa
tunaowafuga.
Wanyama hawa huishi katika vichaka
na sehemu majani makavu makavu, hubeba mimba kwa miezi mitatu na siku chache
kidogo kama atazidisha, na hawana idadi maalumu ya watoto anaozaa hapa
hutegemea dume lilikuwa na mbavu kiasi gani, lakini kwa kifupi huzaa watoto
wengi, watoto hukaa chini ya uangalizi wa mama kwa kwa miezi mitatu na baada ya
hapo huanza kujitegemea, wanapofikisha mwaka mmoja majike huanza kunusa harufu
ya kuitwa mama, maana huanza kuyadondosha mate madume, kwa muonekano wao mzuri
na wakuvutia.
Viumbe hawa huishi kwa miaka kumi
tuu na wakizidisha wanaweza fikisha miaka 12, huishi kwa kuendeleza koo zao, na
wanafahamiana vyema wapenzi Sana wa kushirikiana, na walinzi wazuri wa mipaka
yao.
Tabia yao ya umoja, kushirikiana huwafanya
waonekane ni wababe wa mji, wanyama hawa huogopwa hata na wanyama wenzao wanao
winda kwani bifu lao huwa ni lakufunga mtaa, hata simba akiwaona mkia wake
huuficha, usiseme kwa fisi nk, huweza kukimbia umbali wa km 71 kwa saa, hivyo
kaa ukijua ni viumbe ambao wana hatari sana wakati mwingine humla mnyama wakati
wanamkimbiza.
Mbwa mwitu wapo wa aina mbili
ninaowafahamu wapo hawa ninaowazungumzia ambao kwa lugha ya mama Theresa
wanaitwa wild dog, na wapo aina nyingine wanaitwa wolf, tulio nao hapa nyumbani
ni hawa wild dog, wolf hatuna katika mbuga zetu.
Tofauti yao huanzia katika
muonekano, mbwa mwitu wa kwetu ni wadogo sana katika maumbo, wakati wolf ni
mbwa mwitu wakubwa sana pengine kuliko tunaowafuga, mbali na muonekano lakini
pia majuku yao hufanya kwa staili tofauti, wakati mbwa wa kiAfrika wanapokwenda
kuwinda wakiongozana pamoja na kufukuza pamoja windo lao, wolf hugawana njia na
mmoja wao anapoona windo huanza kwa kulizubaisha akilikenulia meno na kutoa
sauti ambayo wenzao hutambua kuwa wanaitiwa nini, wolf ni mnyama anayevutia na
anamuonekano mzuri sana na rangi zao ni nzuri sana ukimuona unaweza tamani
umkumbatie lakini roho yake ni ya kinyama sana hana huruma hata chembe ni heri
ukutane na simba, mbwa mwitu wetu wana sura mbaya hawana rangi nzuri lakini kwa
binadamu wana utu sana hawezi kukuvamia pasina sababu, wakati wolf ni viumbe
ambao kwa mbio wanaweza fata kwa duma, ndio kwanza mbwa mwitu wetu hawana mbio
sana.
******************VYAKULA
WANAVYOPENDELEA **********************
Mbwa mwitu ni wanyama wanaokula
nyama na wanyama wanaopendelea kuwawinda ni pamoja na paa, mbawala,
nyumbu,pundamilia nk pamoja na wanyama hao lakini pia huweza kuwawinda wanyama
wakubwa ambao hata simba huwaogopa kama nyati na twiga nk. Mbali na nyama
vijamaa hivi pia hula matunda ya polini pamoja na majani ambayo hutumia kama
dawa pindi wajisikiapo wagonjwa.
*****************SIFA ZAO ZA
KIPEKEE***********
1. Maisha yao ni mpela mpela,
hakunaga muda wa kupumzika muda wa kazi kila kitu ni mchaka mchaka tuu,
wanaharaka pasina mfano.
2. Wanaamini katika ujamaa
3. Ni marufuku kujipaka damu wakati wa kula, na atayepatikana na damu wenzie humtafuna pia.
4. Wanapokula hunyofoa nyama hula, hujifuta damu kisha hufata nyama tena.
5. Wanaokula hutenga chakula cha watoto, sasa wewe na ukubwa wako jalibu kula utaiaoma.
6. Ukimpiga mmoja akakimbia dakika tano nyingi atarudi na kundi na utajuta kuzaliwa, nyati huwa wanaelewa sana kinachowapata kwa sababu ya ubabe wao.
7. Hutu tujamaa huwa hatukubali kushindwa, na kushindwa kwao ni kurudi nyuma kujipanga.
8. Hutambua wanyama wagonjwa na hutumia sana fursa hiyo kuwakamata hasa wale wakubwa kama nyati na twiga.
9. Ukiwaonesha damu ni kama umewaharibu akili hapo hawatajali ww ni nani, binadamu, simba , chui, nyati ukianguka ndio wanaridhika.
10. Ni wanyama ambao hutumia muda mfupi sana kuridhishana kimapenzi, dakika chache tuu Biashara imeisha na kibend juu.
11. Huwaficha watoto wao wasiwaone wawapo katika mahaba, cha ajabu watoto wao mwaka mmoja tuu nao huanza kufanya waliyokuwa wamefichwa sasa sijui wanajifunzia ndotoni.
12. Staili wanayotumia kula hata wanyama wanaokula nyama huishia kuwatizama tuu, na hakuna anayeweza kuwasogelea hata kama ana njaa, fisi huwa anachekaa weeee mpaka anaamua akafanye kazi nyingine.
13.wakishiba muda wao mwingi hutumia katika michezo, mfano kupigana , kukimbizana nk.
14. Kachezee chochote alichonacho Ila ukitaka ubaya naye kaguse watoto wake na kama kamoja kambeya kapige kelele, jicho utalopigwa litasadifu unachokwenda kufanywa.

15. Jike hupandwa na dume mbabe,
hivyo wanyonge wa mwisho huenda kutafuta majike katika koo zingine na huo
huweza kuwawinda mwanzo wa kuanzisha jamii yao mpyaa.
****************UKIKUTANA NAO UFANYE
NINI ****************
Inasemekana viumbe hawa pamoja kwamba ni wapenzi wa nyama lakini hawanaga neno na mwanadamu, humuheshimu kama mbwa anaowafuga wanaomuheshimu, sasa basi heshima unayopewa itumie vizuri, sio unaanza kuleta tabia zetu za kiswahili ukiona mbwa unaokota jiwe na kumtupia, hawa jamaa hawapendagi dharau, lakini pia hakikisha hauna sehemu inayovuja damu kwani wakiisikia tuu wafyaa ! wakati huo endelea kufanya jitihada za kupotea maeneo hayo, maana ni binadamu tuu ndiyo amepewa ufahamu timilifu japokuwa naye hujichetua inapobidi.

*************MWISHO ***************

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni