Mbunge wa zamani wa jimbo la kilombero kupitia ccm Abdul mteketa amefanyiwa upasuaji leo katika taasisi ya tiba ya mifupa na mishipa ya fahamu muhimbili MOI kutokana na tatizo la magoti linalomsumbua.
mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma na ustawi wa moi almas juma amesema mteketa alifikishwa hospital hiyo februari 11,2018 anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji leo februari 14 ,2018
''amefanyiwa upasuaji anaendelea vizuri mengine kuhusu ugonjwa atawajulisha lakini kwasasa bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari ''amesema jamaa
mbali na kuwa mbunge wa jimbo la kilombero , mteketa pia ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu katika vilabu vya simba ,pan africa . hivi karibuni alikaririwa na vyombo vya habari akisema ameugua kwa muda mrefu tangu akiwa mbunge wa jimbo la kilombero .
mbali na hilo mteketa amemshukuru rais magufuli kwakumsaidia matibabu yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni