Jumapili, 25 Februari 2018

Manchester United yarejea nafasi ya pili, yaichapa Chelsea 2-1

Manchester United imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Chelsea inayonolewa na Kocha, Antonio Conte katika mchezo wa Ligi Kuu Soka nchini England uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Old Trafford.

Mbrazil Willian aliwapa uongozi wageni Chelsea dk 32 ya kipindi cha kwanza kabla ya mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Romelu Lukaku kuisawazishia Manchester United dk 39 ya kipindi cha kwanza na kinda Jesse Lingard kumuahikikishia Kocha, Jose Mourinho pointi tatu baada ya kuusindikiza wavuni mpira dk ya 75.

Kwa matokeo hayo Manchester United imefikisha pointi 59na kurejea katika nafasi yake ya pili nyuma ya vinara Manchester City walio na alama 72 wakati Liverpool ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya West Ham jana wakirudi katika nafasi yao ya tatu na alama zao 57.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni