Pep Guardiola amefanikiwa kuiongoza Man City dhidi ya Arsenal kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ambayo yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 18, Vincent Kompany dakika ya 58 na goli la mwisho likafungwa na David Silva dakika ya 65.
Kutwaa taji hilo kwa Man City kunawafanya wafikishe jumla ya mataji matano ya Kombe la Ligi, huku Liverpool ikisalia kama club pekee England iliyowahi kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ya timu zote ikitwaa mara nane, Arsenal wao leo wanakuwa wamepoteza fainali yao ya sita ya Kombe la Ligi kati ya fainali nane walizowahi kucheza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni