Alhamisi, 22 Februari 2018

JUHUDI KAZINI

Image may contain: 1 person, sleeping, baby and closeup


Mtangazaji wa Redio wa kipindi cha Asubuhi nchini Marekani amejifungulia studio wakati akiendesha kipindi chake hicho.

Cassiday Proctor, mtangazaji wa vipindi vya kila siku vya asubuhi katika Kituo cha Redio cha The Arch kilichopo kwenye mji wa St Louis, Marekani alitangaza kipindi chake hicho Jumanne wakati akifanyiwa upasuaji.

Mtangazaji Proctor alianza kuyasikia maumivu ya uchungu mwanzoni mwa juma hili, na hivyo kufanya maandalizi kwa msaada wa kituo anachofanyia kazi pamoja na hospitali aliyopaswa kujifungulia kwaajili ya kurusha hewani tukio hilo.

Mwanamama huyo ameiambia BBC kuwa ulikuwa ni muda adhimu kutumia fursa hiyo kutangaza wakati mwanaye akitolewa tumboni huku zikiwa zimesalia Juma mbili kutimu muda wa mtoto kuzaliwa..

"Ni furaha ya kipekee kuzungumzia uzoefu wangu katika tukio hili adimu na la kufurahisha kwenye maisha yangu na wasikilizaji wa redio yetu," alisema Proctor wakati wa kipindi chake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni