Ilianzia Dodoma pale ambapo alipatika mtoto aliyejulikana kwa jina la Ajib wa Dodoma kuandika tshirt yake kwa peni jina la Ajib na namba lakini wakati huu ni wakati wa Okwi wa Bukoba ambaye leo amekabidhiwa jezi za shujaa wake Emmanuel Okwi.
Leo mtoto Shabani Okwi ambaye ni shabiki wa mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi ambaye picha zake zilisambaa akihojiwa na Azam TV akiwa ameandika jina la Okwi kwenye nguo yake, amekabidhiwa jezi ya shujaa wake Okwi na kiongozi wa Makundi ya Simba mtandaoni Jose Munyama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni