Rais John Magufuli leo Februari, 16 amewaapisha mabalozi wawili
aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.
Mabalozi walioapishwa ni pamoja na Muhidin Ally Mboweto ambaye
ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Dkt. Wilbrod Peter
Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana Februari, 15.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni