
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu usiku huu baada ya shinikizo kubwa kutoka kwenye chama chake cha ANC.
Bunge la Afrika Kusini lilikuwa lipige kura ya kutokuwa na imani na Zuma asubuhi ya Alhamisi, kura hiyo sasa haitapigwa tena.
Kiongozi wa ANC na Makamu wa Rais Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wa nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika.
Zuma ametangaza hadharani kujiuzulu kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambapo amesema asingependa damu imwagike na chama ANC kimeguke kwa sababu yake.
Uamuzi wa Zuma umekuja kutokana na msukumo uliokuwa unatolewa na Chama chake pamoja Bunge la nchi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni