

Abiria takribani 66 wanahofiwa kufa kufuatia kuanguka kwa ndege yenye safari namba EP3704 iliyotokea Tehran nchini Iran. Inaelezwa kuwa iliangukia katika maeneo ya milima ya Zagros karibu na mji wa Semirom kwenye Jimbo la Isfahan katikati ya mji wa kusini magharibi mwa mji wa Yasuj, vyombo vya habari vimeripoti.
Hata hivyo inadaiwa kuwa hali mbali ya hewa inasababisha ugumu kwa helkopta kufika katika eneo hilo la ajali.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya majeruhi iliyowekwa wazi.
"Vikosi vyote vya dharura viko kwenye tahadhari," msemaji wa huduma za dharura amesema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni