Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za ajali mbaya ya ndege iliyotokea leo karibu na mji mkuu wa Urusi Mosco ambapo abiria wote na wafanyakazi wa ndege waliokuwemo wamearifiwa kupoteza maisha.
Kupitia
taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Guterres ametuma salamu za
rambirambi kwa familia za wafiwa, watu na serikali ya shirikisho ya
Urusi.
Kwa mujibu wa duru za habari ndege hiyo ya shirika la ndege la Saratov ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo na kuanguka kwenye mji wa Ramenskoye karibu na Mosco ikikatili maisha ya watu wote 71 waliokuwemo wakijumuisha abiria 65 na wafanyakazi wa ndege 6.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni