Jumamosi, 20 Januari 2018

Waziri Mwakyembe baada ya amekutana na Rais wa Simba leo



 jumamosi ya January 20 2018 waziri wa habari utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amekutana na kaimu wa Rais wa Simba na katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao kujadilii mambo kadhaa kuhusiana na mfumo wa mabadiliko wa club ya Simba.
Dr Mwakyembe ameongea na vyombo vya habari baada ya kufanya mkutano na kaimu Rais wa Simba na kuelekeza kuwa mfumo wa hisa wanaoingia na muwekezaji wake wanapaswa kufuata na kuheshimu utaratibu na kanuni za BMT ikiwemo muwekezaji kupata asilimia 49 na wanachama asilimia 51.
“Kwa kipindi kirefu serikali imekuwa katika mchakato wa kutengeneza kanuni zinazoweza kusimamia uwekezaji katika michezo yetu hapa nchini na hii imetokea baada ya serikali kuona michezo yote ikiwemo soka maendeleo yake yanategemea pesa”>>>DR Mwakyembe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni