Ijumaa, 26 Januari 2018

#VPL KIYOMBO APEWA ZAWADI YAKE


Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea muda huu kwa mchezo mmoja unaopigwa katika dimba la Mabatini mkoani Pwani kati ya Ruvu Shooting na Mbao FC.
Kabla ya mchezo huo kuanza, mchezaji wa Mbao FC Habib Haji Kiyombo amekabidhiwa zawadi yake ya mchezaji bora wa mwezi Desemba 2017.
Zawadi hizo ni Tuzo maalum, King'amuzi cha Azam TV pamoja na mfano wa hundi ya shilingi milioni moja.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni