Jumamosi, 20 Januari 2018

Vanessa Mdee amezindua ‘app’ ya simu ya Vee Money



Muimbaji wa Bongofleva Vanessa Mdee kesho Jumamosi ya January 20 2018 ndio CD za abum yake ya Money Mondays zitakuwa zinatoka, leo January 19 tumeipokea good news nyingine kutoka kwake kwa ajili ya mashabiki wake, huu ni mfululizo wa matukio ya kihistoria katika muziki wa Vanessa Mdee.

Good News ikufikiea kuwa leo Vanessa Mdee amezindua programu ‘app’ yake mpya ya simu itakayokuwa inajulikana kwa jina la VEE MONEY ambapo itakuwa inapatikana bure kupitia ‘Google Play store’ na ‘Apple store’, wiki ya kihistoria ya Vanessa itakamilika kesho Mlimani City DSM kuanzia saa 4 asubuhi hadi 12:00 jioni.

Programu hii imetengenezwa na kampuni ya masuala ya teknolojia ya Marekani Converge Media, lengo likiwa ni kutengeneza sehemu ambayo mashabiki wa Vanessa watakuwa wanapata ya kusikia/kuona video, nyimbo, picha na kurasa za kijamii za muimbaji Vanessa  Mdee.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni