Jumamosi, 20 Januari 2018

UONAPO DALILI HIZI CHUKUA HATUA

Serikali imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya Chikuganya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea jijini Mombasa nchini Kenya.
Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu imesema kuwa mpaka sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado halijatoa taarifa rasmi lakini kama nchi wameona ni vyema wakatoa tahadhari ya kuzingatiwa kwa muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchi hizi mbili za Kenya na Tanzania.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya wanasema, ugonjwa wa Chikunganya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu aina ya Aedes na kusema ugonjwa huo siyo mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi kutokea katika maeneo ya kusini huko Makonde mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari imezitaja baadhi ya dalili za wagonjwa huo kuwa ni pamoja na homa kali, kuumwa kichwa, maumivu ya kichwa na uchovu, kichefuchefu na kizunguzungu na wakati mwingine tumbo kuuma.

 No automatic alt text available.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni